Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

  1. Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo ya moja kwa moja ya ukurasa wa BBC Swahili...Shukrani

  2. Mwandishi asimamishwa kazi kwa kashfa ya kutoa taarifa potofu

    m

    Kusimamishwa kazi kwa mwanahabari wa cheo cha juu katika kituo cha habari cha TV cha Ufaransa kumefichua kile kinachoonekana kuwa mfumo mzuri wa rushwa na ushawishi wa kununua katika vyombo vya habari vya kimataifa.

    Iliripotiwa mnamo Januari kwamba Rachid M'Barki mwenye umri wa miaka 54, mwandishi mkongwe anayeheshimika wa BFM, alikuwa ameondolewa katika majukumu yake ya utangazaji kwa muda mfupi akisubiri uchunguzi wa kina juu ya madai yanayomkabili ambao ulikuwa wa siri.

    Lakini sasa uchunguzi wa gazeti la Le Monde kwa kushirikiana na shirika la kampeni la Forbidden Stories umefichua maelezo zaidi.

    Kwa mujibu wa uchunguzi huo, M'Barki alifanya uchunguzi wa juu ya mada mbalimbali kama vile boti za kifahari huko Monaco, kiongozi wa upinzani wa Sudan, madai ya rushwa nchini Qatar ambayo yote yalikuwa na kitu kimoja: yaliyohusu Israeli katika 'habari za kukodisha'.

    M'Barki amekanusha kulipwa ili kufanya taarifa hizo lakini anakiri kukwepa ukaguzi wa uhariri wa BFM.

    Anasema alipewa ripoti hizo na mpatanishi na alitumia uamuzi wake wa kitaalamu katika kuchagua kuzitumia.

    Lakini wachunguzi hao wanasema wana ushahidi kwamba chanzo cha habari hizo linatokana na kundi la Team Jorge, operesheni yenye makao yake mjini Tel Aviv na inayoendeshwa na afisa wa zamani wa kikosi maalum cha Israel ambaye jina lake halisi ni Tal Hanan.

  3. Mbu hatari agunduliwa Kenya-Utafiti

    mbu

    Watafiti nchini Kenya wamegundua mbu kutoka Asia ya Kusini ambaye anayeua wadudu wanaopatikana barani Afrika.

    Timu ya wataalam wa wadudu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu ya Kenya imebaini mbu anayekaa jiji hilo anayejulikana kama Anopheles Stephensi wakati wa zoezi la uchunguzi wa kawaida katika kaunti ya Marsabit, kaskazini mwa Kenya.

    "Kwa bahati mbaya, ugunduzi huu nchini Kenya unaweza kutafsiriwa kwa kiwango cha juu cha maambukizi ya malaria katika maeneo ya mijini na kando ya miji nchini humo na inaweza kubadilisha mafanikio yaliyopatikana katika vita dhidi ya malaria.

    " Dkt Samuel Kariuki, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kenya Medical Research alisema kwenye taarifa. Mbu huyu anaweza kusababisha maambukizi zaidi kwani hustawi katika msimu wa mvua na kiangazi.

    Visa vingi vya malaria katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara huripotiwa wakati wa msimu wa mvua.

    Watafiti wanatoa wito kwa Wakenya kutumia zana zinazopatikana za kudhibiti malaria kama vile kulala chini ya vyandarua vilivyotibiwa kwa dawa na kuvaa nguo za mikono mirefu ili kuzuia kuumwa na mbu.

    Pia wameanza kumtafuta mbu huyu katika maeneo yasiyo ya kawaida mfano vyombo vya maji kwani anaweza kuzaliana popote.

    Mbu huyo aligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Djibouti miaka kumi iliyopita na sasa ameonekana Ethiopia, Sudan, Somalia na Nigeria.

    Soma zaidi:

  4. China inaweza kuipa silaha Urusi kwa ajili ya vita vya Ukraine

    china

    China inafikiria kumpa Urusi silaha kwa ajili ya vita vya Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken amesema.

    Bw Blinken aliiambia CBS News kwamba kampuni ya China tayari ilikuwa ikitoa "msaada wa kijasusi" kwa Urusi na habari mpya ziinaeleza Beijing inaweza kutoa "msaada wa silaha".

    Hii ikiwa ina maana kuwa athari itakuwa kubwa zaidi" China, imeonya.

    China imekanusha ripoti kwamba Urusi imeomba vifaa vya kijeshi.

    Rais wa China Xi Jinping ni mshirika wa Rais wa Urusi Vladimir Putin na bado hajalaani uvamizi wa Urusi lakini ametaka kutoegemea upande wowote katika mzozo huo na ametoa wito wa amani.

    Bw Blinken alikuwa akizungumza na CBS baada ya kukutana na mwanadiplomasia mkuu wa China, Wang Yi, Jumamosi katika Mkutano wa Usalama wa Munich.

    Alisema wakati wa mkutano huo alionesha "wasiwasi mkubwa" juu ya "uwezekano kwamba China itatoa msaada wa silaha mbaya kwa Urusi".

    "Hadi sasa, tumeona makampuni ya China... yakitoa usaidizi usio na madhara kwa Urusi kutumia nchini Ukraine.

    Wasiwasi tulio nao sasa unatokana na taarifa tulizonazo kwamba wanafikiria kutoa usaidizi wa silaha," alisema.

    Hakufafanua ni taarifa gani Marekani imepokea kuhusu mipango ya China.

    Soma zaidi:

  5. Mkutano baina ya viongozi wa China na Marekani wazidisha mzozo wa Puto

    m

    Wakati mzozo baina ya Marekani na China ukiongezeka kuhusu puto za kijasusi, na ndivyo mgawanyiko ulivyoongezeka baina ya jumuiya ya kimataifa unaokagua hali katika mzozo huo.

    Majibizano mengine makali yaliibuka Jumamosi wakati Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alipokutana na Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi kando kando mwa mkutano wa usalama wa Munich katika mkutano wa kwanza wa kiwango cha juu tangu kuzuka mzozo huo.

    Blinken amesema "hatutakubali ukiukaji wowote wa uhuru wetu" na kusema kwamba " hatua hii ya kutowajibika ni lazima isitokee tena". Wang, kwa upande wake alitaja mkasa huo kama "uongo wa kisiasa uliozushwa na Marekani" na kulishutumu taifa hilo kwa "kutumia nguvu zote kuizuia na kuikandamiza China".

    China inaendelea kukana kuwa ilituma puto la kijasusi, hata wakati Marekani inaendelea kubaini taarifa zaidi kuhusu kifaa hicho kuthibitisha tuhuma zake.

    Lakini zaidi ya mzozo huo namna ambayo Beijing na Washington zimejibizana ni jambo ambalo limetazamwa kwa makini wakati dunia ikitafakari tukio hilo na athari zake kwa usalama wa kitaifa na utulivu wa kisiasa wa kieneo.

    Matokeo yake waangalizi wanasema ni kwamba imefanya misimamo kuwa thabiti, kuongeza kutoaminiana miongoni mwa wale wanaozitazama China au Marekani na kufanya kuwa vigumu zaidi kwa Washington na Beijing kuziba pengo baina yao.

    Soma zaidi:

  6. Mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli ya 'Tour du Rwanda' yameanza Rwanda

    Yves Bucyana

    BBC Swahili

    rwanda

    Mzunguko wa kwanza wa mbio za Tour du Rwanda, umeshirikisha waendesha baiskeli 93 kutoka timu 20, zikiwemo zile za Afrika na mabara mengine kama Ulaya, waliondoka Kigali na kuelekea Rwamagana mashariki mwa Rwanda, umbali wa kilomita 115.6.

    m

    Huku muingereza Ethan Vernon, anayechezea timu ya Soudal Quick Step, alishinda mzunguko wa kwanza wa mbio za kimataifa za baiskeli za Tour du Rwanda - Ethan Vernon mwenye umri wa miaka 22, ambaye kwa kawaida hushiriki mashindano makubwa katika bara la Ulaya, alitumia muda wa saa 2 dakika 45 na sekunde 52 kutoka Kigali hadi Rwamagana umbali wa kilomita 115,6 lakini pia washindani walizunguka mara tano katika barabara za mji huo.

    Muingereza Chris Froom ameshika nafasi ya 44 lakini ametumia muda usiotofautiana na muda uliotumiwa na mshindi Ethan Vernon. Kesho, waendesha baiskeli katika mzunguko wa pili kutoka Kigali hadi Gisagara kusini mwa Rwanda , umbali wa kilomita 132.9.

    Mnamo 2019, mashindano ya Tour du Rwanda yalitoka kwenye kiwango cha 2.2 hadi kiwango cha 2.1 cha mashindano yalioyoko kwenye kalenda ya shirikisho la kimataifa la mbio za baiskeli UCI.

    m

    Miongoni mwa timu kubwa zinazopewa nafasi kushinda mbio hizi ni Totalenergy kutoka Ufaransa, Green Project kutoka Italia, Eritrea na Israel Premier Tech, ambayo inashirikisha nyota wa kimataifa wa mbio za baiskeli muingereza Chris Froome.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 ameshinda Tour de France mara 4, Giro Italia mara 1 na Tour d'Espagne mara 2.Japo mara hii anashiriki mbio za baiskeli kama kujifurahisha.

    Mashindano haya pia yanajumuisha waendeshabaiskeli 2 ambao wameshinda Tour du Rwanda ilipokuwa ya kiwango cha 2.2, ambao ni Mnyarwanda Jean Bosco Nsengiyumva mnamo 2015 na Mueritrea Daniel Teklehaimanot aliyeshinda 2010.

    Soma zaidi:

  7. Korea Kaskazini yarusha makombora baada ya kutishia kulipa kisasi

    m

    Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa marefu (ICBM) siku ya Jumamosi katika mazoezi ya "yaliyoshangaza watu" ili kuthibitisha kutegemewa kwa silaha hiyo, vyombo vya habari vya serikali vilisema.

    Liliruka zaidi ya kilomita 900 (maili 560) kwa dakika 67 na kutua katika Bahari ya Japani.

    Korea Kaskazini ilisema jaribio hilo lilionesha kuwa lina uwezo wa kukabiliana na vikosi vya uadui kama vile Marekani na Korea Kusini.

    Hatua hii inakuja kabla ya mazoezi ya pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini hapo mwezi ujao, kukabiliana na vitisho vya nyuklia vinavyoongezeka vya Korea Kaskazini.

    Mamlaka ya Korea Kaskazini yametishia kulipiza kisasi "kwa nguvu isiyo na kifani" kwa mazoezi yoyote kama hayo - ambapo inasisitiza kuwa yanafanywa ili kujiandaa kuivamia Korea Kaskazini.

    Suala hili lilitekelezwa mapema Jumapili na Kim Yo-jong, dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, ambaye alisema vitendo vyovyote vya uhasama vitakabiliwa na jibu "kali na kubwa".

    Pia aliitaka Marekani kukomesha kile alichokiita "vitisho" dhidi ya serikali.

    Lakini aliongeza kuwa mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul, hautalengwa na makombora ya Korea Kaskazini.

    Siku ya Ijumaa, Korea Kaskazini ilionyesha uwezo wake mkubwa wa kijeshi katika gwaride.

    Soma zaidi:

  8. Mwanadiplomasia wa Israel aondolewa kwenye mkutano wa AU

    m

    Mwanadiplomasia wa Israel Bi. Sharon Bar-li aliondolewa katika mkutano wa wakuu wa nchi wa Umoja wa Afrika kwa kuwa hakuwa mtu aliyeidhinishwa kuiwakilisha Israel, msemaji wa AU amesema.

    Video inayosambaa mtandaoni inamuonesha akiondolewa na mlinzi nje ya mkutano nchini Ethiopia.

    Aidha ,msemaji wa Israel ameilaumu Afrika Kusini na Algeria kwa kuondolewa kwake.

    Hadhi ya Israel katika AU imekuwa chanzo cha mvutano.

    "Video inayomuonesha mlinzi akimkaribia mjumbe wa Israel wakati sherehe za ufunguzi wa mkutano wa mwaka zikiendelea.

    Kulikuwa na majadiliano na Bi Bar-li, ambaye ni naibu mkurugenzi mkuu wa Afrika katika wizara ya mambo ya nje ya Israel, kisha akaondoka pamoja na mlinzi.

    "Israel inaliangalia tukio hilo kwa umakini ambapo... Balozi Sharon Bar-li, aliondolewa kwenye ukumbi wa Umoja wa Afrika licha ya wadhifa wake na kuwa na beji ya kuingia," msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lior Hayat amenukuliwa na gazeti la Times of Israel akisema. .

    Kisha aliilaumu Algeria na Afrika Kusini kwa kuhusika na hatua hiyo, akiongeza kuwa "zinaendeshwa na chuki"

    Lakini afisa wa AU amesema Bi Bar-li "aliombwa kuondoka" kwa kuwa hakuwa amealikwa na mkutano huo ulikuwa kwa waalikwa pekee, mualiko alipewa balozi wa AU wa Israel Aleli Admasu, shirika la habari la AFP linaripoti.

    "Inasikitisha kwamba mtu anayehusika angetumia vibaya uungwana kama huo," AFP inamnukuu afisa huyo ambaye hakutajwa jina akisema.

    Soma zaidi:

  9. Habari za Jumapili...Karibu katika ukurasa wa moja kwa moja wa BBC Swahili leo ikiwa tarehe 19.02.2023