Virusi vya Corona: Mama yake meneja wa Manchester City Pep Guardiola afariki kutokana na corona

Mwezi uliopita, Guardiola alitoa mchango wa euro milioni 1 sawa na pauni 920,000 kwa jili ya kusaidia katika vita dhidi ya mlipuko wa virusi vya corona.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwezi uliopita, Guardiola alitoa mchango wa euro milioni 1 sawa na pauni 920,000 kwa jili ya kusaidia katika vita dhidi ya mlipuko wa virusi vya corona.

Mama yake Meneja wa timu ya Manchester City Pep Guardiola, amefariki dunia mjini Barcelona akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.

"Washirika wa klabu hiyo wamemua wakituma ujumbe wa sambi rambi katika kipindi hiki kigumu kwa Pep, familia yake na marafiki zake wote ," umesema ujumbe wa timu ya Manchester City uliotumwa kwenye mitandao ya kijamii.

Ongezeko la Jumatatu la vifo 637 vya virusi vya corona linamaanisha kuwa hadi sasa watu 13,055 wamekwishakufa nchini Uhispania kutokana na janga hilo.

Mwezi uliopita, Guardiola alitoa mchango wa euro milioni 1 sawa na pauni 920,000 kwa jili ya kusaidia katika vita dhidi ya mlipuko wa virusi vya corona.

Pesa hizo zitatumika katika kununulia vifaa vya matibabu na kujikinga na maambukizi kwa ajili wahudumu wa tiba wanaowashughulikia wagonjwa waliolazwa hospitalini.

Taarifa za corona

Chanzo cha picha, Taarifa za corona

Taarifa zaidi juu ya virusi vya corona kuhusu spoti:

Barcelona iko katika jimbo la Catalonia, ambako ni moja ya maeneo nchini Uhispania yenye idadi kubwa ya visa vya corona.

Manchester United ilituma ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii ikisema klabu hiyo "imesikitishwa sana kusikia taarifa hii mbaya ", na kuongeza kuwa: "Tunatuma rambirambi zetu kwa Pep na familia yake ."

Guardiola ambaye ni Mhispania, mwenye umri wa miaka , 49, amekua meneja wa Manchester City tangu mwezi Julai 2016 baada ya kuhudumu kama meneja katika timu za Barcelona na Bayern Munich.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?